Archives

 

                                          Ndoa Na Nyumba

Baadhi ya warembo waliojitokeza katika sherehe za
wapendanao duniani wakiwa kwenye picha ya pamoja na mrembo bora.Aliyevaa taji kushoto ni mrembo bora wa mwaka 2007, wakati katikati ndiyo mrembo bora mwaka 2008. Picha na Pius Teneng/AjabuMedia

NA KENNEDY SIYAME,
BOSTON USA.

02/29/2008

Kushindwa kujipendekeza na kuona aibu ya kuwanyenyekea waume zao  kwa wanawake wengi waliojaliwa kuingia katika ndoa,kumetajwa kuwa ni chanzo kimojawapo kikubwa kinacho haribu  uhusiano wa wanandoa kimapenzi, na hatimaye Kupelekea ndoa zao kuvunjika na kusababisha madhara makubwa katika nyumba.

Rai hiyo imetolewa na Nabii mwanamke Bibi.Mwaka Twagirayesu wakati wa mahubiri yake katika sherehe za wapendanao duniani(valentineday)  zilizofanyika katika mji wa Chelmsford, MA, .kwenye hoteli ya kifahari ya Radisson na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka barani Afrika,Marekani na Ulaya.

Katika mahubiri yake yaliyojaa mahusia kwa wanandoa,vijana wa kiume na mabinti,Bibi.Mwaka alisema ndoa inamisingi yake ambayo ikilindwa na kuhifadhiwa kisawasawa,wanandoa wanaweza kujikuta kanakwamba wanaishi peponi na kwamba huo ndio mpango halisi wa Mungu wa kuanzisha ndoa.

“Nataka niwaambie mabibi na mabwana, kwamba hupungukiwi kitu kujipendekeza kwa mumeo,mimi hua najipendekeza sana kwa mume wangu, kama ametoka najua wakati wake wa kurejea nyumbani na unapofika wakati huo naweza hata kukaa mlangoni nikimsubilia”alisema Bibi.Mwaka huku akionesha hali ya kutamba akiwa madhabahuni.

Alisema kwa mujibu wa neno la Mungu, Biblia katika kitabu cha Efeso5:22 imeonesha wazi kwamba wajibu wa mwanamke ni kutii(kumtii mume wake)wakati mwanaume ameagizwa kupenda (kumpenda mke wake) na kwamba kila mmoja akiwajibika kwa nafasi yake, matatizo ya ndoa hayataweza kutokea kamwe.

Kwa mujibu wa Bibi.Mwaka matatizo mengi yanayojitokeza katika ndoa nyingi za kikristo na zisizo za kikristo, ni kutokana na wanandoa wengi kushindwa  kulitii neno la Mungu na kuamua kuishi kwa kuendesha ndoa zao kwa kutumia akili, mali pamoja na sheria za nchi hali ambayo hupelekea taraka na watoto wa mitaani.Watu wengi kutokana na kushindwa kutii neno la mungu, hufurahia ndoa na kushindwa kufurahia nyumba.

“Mungu ndiye mwanzilishi wa Ndoa, nayeye kama msingi wa mambo ya ndoa na nyumba hawezi kusimama kwenye mabadiliko ya sheria za nchi ili kutafuta ulinganifu kati ya mume na mke”alisema Bibi.Mwaka na kuongeza “mume ataendelea kuwa kichwa cha nyumba siku zote wakati mke akiendelea kuwa mtii”.

Awali kabla ya mahubiri yake Bibi.Mwaka,sherehe hizo  zilitanguliwa na burudani ya muziki tofautitofauti ambapo watu kutoka katika mataifa mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo ya wapendanao duniani walicheza kwa mujibu wa mitindo ya nchi zao.(Angalia picha)


Baadhi ya warembo ambao bado hawajaolewa kwenye mitindo ya mavazi wakisakata muziki baada ya kupewa nafasi ya pekee ya kujitangaza katika sherehe ya wapendanao duniani. H.Maina/AjabuMedia

Baadhi ya washiriki wa sherehe za wapendanao duniani wakiwakilisha mataifa yao namna ya kucheza mziki katika mitindo mbalimbali ambapo taifa la Kenya liliibuka kuwa mshindi. H.Maina/AjabuMedia

Sherehe hizo,pia zilipambwa kwa vyakula vya aina mbalimbali lakini kivutio zaidi kilikuwa ni warembo ambao walijitokeza kwa mitindo ya aina aina ya mavazi pamoja na mapambo  ambao kabla ya hitimisho walifanyiwa maombezi maalumu ili wapate wenzi wa maisha yao kutoka kwa Mungu.

Aidha warembo hao  pia walipata muda maalumu wa kuuliza maswali ambapo swali lililotoa changamoto ni namna ya kumjua mume au mke wa kweli kutoka kwa Mungu swali ambalo lilizua utata mwingi kwa kila jibu lililotolewa.Katika sherehe hizo mwanamke kutoka Haiti (ambaye kwa bahati mbaya jina lake halikufahamika mara moja ) alivishwa taji ya kuwa mrembo bora wa mwaka 2008.(Angalia picha).


Kulia ndiye aliyevikwa taji ya mrembo bora wa sherehe za wapendanao duiani mwaka wa 2008 akikumbatiwa kwa furaha na mrembo bora mwaka wa 2007. H.Maina/AjabuMedia

Kwa mujibu wa historia ya sherehe hizo, Bibi.Mwaka na mume wake mtume Darius Twagirayesu wametajwa kuwa ndio waanzilishi wa kuandaa na kuwakusanya mataifa mbalimbali hususani kutoka barani Afrika ambapo katika mwaka huu wameshirikiana na Taifa la Kenya kuandaa sherehe hizo.

Kwa maoni ya mwandishi ya makala hii, kuna tofauti kubwa kati ya ndoa na nyumba ambapo ndoa ni tendo la kujamiana kimwili wakati nyumba ni maisha ya kila siku ndani ya wanandoa. Kwamba kuna umuhimu wa kuwepo mawasilano kati ya mume na mke, watoto na wazazi, familia na mungu..
MWISHO.   


                             Valentines Gala Photo Gallery (Enlarge Album for a full view)

 

  

 

 

  

   

 

 

                                                  





 



 




   


 


 

 



 

 

 

 

 

 

 

 

 


 

 

 
 

Post Your Comments Here
Tell A Friend

 

Flags and Colors of the East African Community

KENYA

UGANDA

TANZANIA

RWANDA

BURUNDI

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 
» Business Directory » Previous Page » Search the WWW » Local Weather » Headline News » Travel » Games » Advertise
» Employment » Privacy Policy » Disclaimer/Terms of Use » Add A Site/Link » Merchant Services » Contact Us » Site Map
©2007 ajabuafrica.com. All rights reserved.